Sanidi viendelezi, programu, na vyanzo vya kusakinisha hati

Hukuruhusu kubainisha ni URL gani zinaruhusiwa kusakinisha viendelezi, programu, na mandhari.

Kuanzia Google Chrome 21, ni vigumu zaidi kusakinisha viendelezi, programu, na hati za watumiaji nje ya Duka la Chrome kwenye Wavuti. Awali, watumiaji wangebofya kiungo cha faili ya *.crx, na Google Chrome ingejitolea kuisakinisha faili baada ya maonyo machache. Baada ya Google Chrome 21, faili kama hizo lazima zipakuliwe na kuburutwa kwenye ukurasa wa mipangilio wa Google Chrome. Mipangilio hii huruhusu URL mahususi kuwa na mtiririko wa zamani na rahisi wa usakinishaji.

Kila kipengee katika orodha hii ni ruwaza ya mtindo wa kiendelezi unaolingana (angalia https://developer.chrome.com/extensions/match_patterns). Watumiaji wataweza kusakinisha vipengee kwa urahisi kutoka kwenye URL yoyote inayolingana na kipengee katika orodha hii. Maeneo yote mawili ya faili ya *.crx na ukurasa ambapo upakuaji utaanzia (yaani kielekezi) lazima viruhusiwe na ruwaza hizi.

ExtensionInstallBlacklist inapewa kipaumbele dhidi ya sera hii. Yaani, kiendelezi kwenye orodha ya kuondoa idhini hakitasakinishwa, hata kama usakinishaji utafanyika kutoka kwenye tovuti ya orodha hii.


Supported on: Microsoft Windows XP SP2 au ya karibuni zaidi
Ruwaza za URL ili kuruhusu viendelezi, programu, na hati za mtumiaji kusakinisha kutoka

Registry HiveHKEY_LOCAL_MACHINE or HKEY_CURRENT_USER
Registry PathSoftware\Policies\Google\Chrome\ExtensionInstallSources
Value Name{number}
Value TypeREG_SZ
Default Value

chrome.admx

Administrative Templates (Computers)

Administrative Templates (Users)